Ijumaa , 30th Nov , 2018

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amezuiwa kusalimiana na mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe alipofika Mahakama Kuu Kanda Maalum ya Dar es salaam hii leo.

Zitto Kabwe akiwa na mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe.

Zitto Kabwe alifika Mahakamani hapo akiwa na viongozi wengine wa CHADEMA ili kushuhudia usikilizwaji pamoja na hukumu ya kesi juu ya dhamana inayowakabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko.

Zitto alionekana kusogea mbele kutaka kumsalimia Mwenyekiti huyo aliyekuwa akisalimiana na baadhi ya watu wengine waliofika mahakamani hapo, lakini yeye aliamriwa kurudi kuketi kwenye nafasi yake.

Hukumu juu ya maamuzi ya kupewa au kutopewa dhamana kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko imeonekana kuwa ngumu baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha ombi la kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa awali wa Mahakama Kuu, ambapo mpaka muda huu kesi bado inasikilizwa.