Ijumaa , 15th Jul , 2022

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewataka wananchi wa mkoa huo kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Makala ametoa kauli hiyo wakati kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani walipofanya ziara za ukaguzi katika vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu. 

RC Makalla ameeleza kuwa ameridhishwa na hali aliyoikuta katika vyanzo hivyo

Lengo la ziara hiyo ni kuangalia hali ya wingi wa maji na kuimarisha ulinzi wa rasilimali za maji. 

Ziara hiyo ilisimamiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira (Dawasa), Mhandisi Cyprian Luhemeja, aliyeambatana na Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya WamiRuvu, Mhandisi Elibariki Mmassi.