
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania, IGP Ernest Mangu
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za jeshi la polisi Mkoani Arusha, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu, amesema kwa mujibu wa uchunguzi ulifanywa na jeshi hilo, wamebaini kwa hatua za awali kuwa bomu lililolipuliwa Aprili 13 mwaka huu majira ya saa 1:30 asubuhi kwenye bara hiyo, ni la kutengeneza kienyeji.
Amesema mbali na bomu hilo kutumika eneo hilo pia wataalamu wa mabomu waliweza kugundua bomu lingine lililokuwa kwenye mkoba ulioegeshwa kwenye kiti katika bar ya Washing Ton ambayo ipo pembeni mwa bar hiyo.
Aidha, majeruhi wa tukio baa ya Night Park waliobaki wodini ni nane na wengine wameruhusiwa, ambao ni Evance Maleko, Evarist Richard, Petro James, Christian Zakaria, Pius Shayo, Antelus Ishengoma, Sudi Ramadhani na Mariam Hansi aliyepo hospitali ya Selian.
Kuhusu kuimarisha ulinzi wakati wa sikukuu za Pasaka amesema kila Mkoa umepewa maelekezo kwa
Kamanda wa polisi watumie mbinu zao zote na vifaa walivyonavyo kama farasi na mbwa walionao, ili kulinda usalama wa ibada za sikukuu hizo.