Jumatatu , 26th Sep , 2022

Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo, amewataka wananchi hasa wazazi kuhakikisha wanazaa watoto ambao watawamudu kuwalea ili kuepusha nchi kuwa na idadi kubwa ya watoto wa mitaani ambao wengine wanaamua kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu ikiwemo panya road.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo

DC Jokate ametoa kauli hiyo leo Septemba 26, 2022, kwenye maadhimisho ya siku ya uzazi wa mpango duniani yaliyoadhimishwa katika hospitali ya Mbagala Rangitatu iliyopo katika Manispaa ya Temeke.