Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 29, 2021, na Waziri wa Maji Jumaa Aweso, wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Halima Mdee, aliyehoji mpango wa Wizara hiyo kutumia utaratibu wa sensa ya watu na makazi ili kupata takwimu halisi ya kila nyumba zinazopata maji.
"Wizara yetu ya Maji inafanya mageuzi makubwa sana tumekutana na watu wa takwimu lakini tunataka tujiongeze mbali badala tu ya kusema asilimia ya watu wanaopata maji twende mbali zaidi tunataka tujue Tanzania kuna vijiji vingapi, vingapi vimepata maji na vipi ambavyo havijapata ili tuhakikishe tunaongeza nguvu maeneo ambayo hayana maji huduma ya maji safi na salama," amejibu Waziri Aweso.


