Jumatano , 23rd Sep , 2020

Wizara ya Maji imeridhika na utekelezaji wa miradi ya maji unaoendelea katika halmashauri ya Manispaa ya mkoa wa Mtwara, baada ya timu ya ufuatiliaji na tathimini kutoka wizarani kufanya ukaguzi wa miradi mkoani humo.

Mkurugenzi wa ubora wa maji Philipo Chandy akikagua maji Mtwara

Timu hiyo kutoka Wizarani iliyoongozwa na mkurugenzi wa ubora wa maji, Philipo Chandy ,akitoa tathmini amepongeza hatua zilizochokuliwa kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa maji huku akikiri kuwa kazi kubwa imefanyika katika manispaa ya Mtwara.

Mkurugenzi Chandy, ameridhishwa na kazi nzuri ya usimamizi wa miradi katika manispaa hiyo unaofanywa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mtwara(MTUWASA).

Aidha Chandy ameitaka MTUWASA kuongeza mtandao ili waweze kutumia vizuri maji katika chanzo cha mtawanya chenye uwezo wa kuzalisha lita millioni 15 kwa siku wakati kwasasa zinatumika lita million 7 pekee kwa siku