Ijumaa , 26th Sep , 2014

Wizara ya kilimo nchini Tanzania inakabiliwa changamoto kubwa ya upatikana wa takwimu za mazao ya Kilimo ambapo kwa sasa hakuna takwimu sahihi ambazo zinaoonyesha usahihi wa mazao ya kilimo nchini Tanzania.

Mazao ya Kilimo Sokoni

Mkurugenzi msaidizi wa idara ya sera na mipango kutoka wizara ya kilimo na chakula Oswadi Rubohe amesema utafutaji wa takwimu za kilimo unaigharimu serikali ambapo ili kupata takwimu za mazao ya kilimo zinahitajika shilingi bilioni 7 hadi kumi 14 za kitanzania kwa mwaka.

Rubohe amewaomba wadau wa maendeleo kusaidia katika kufanya tafiti za mazo ya kilimo ili Tanzania iweze kuwa na takwimu sahihi za mazao .