Mjumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria - LAS Bw. Gideon Mandes (mwenye miwani) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Makundi Maalumu nchini Tanzania wakiwemo watu wenye ulemavu wa macho wamezitaka taasisi zinazotoa msaada wakisheria kuwasaidia ili waweze kupata haki zao katika masula mbalimbali yanayohitaji msaada huo.
Akizungumza na East Africa Radio mjumbe wa bodi kituo cha Sekretarieti ya Msaada wa Sheria LAS Gideon Mandes ambaye pia ni mlemavu wa macho amesema makundi maalumu yanachukua asilimia 10 ya watu wote nchini na kwamba ni vyema watoa msaada wa kisheria kuwa karibu nao ili kutatua kero zao.
Naye Mwenyekiti wa LAS, Mwanasheria Teodosia Muhulo amesema wamefanya utafiti kuhusu msaada wa sheria kwa watu walio katika vizuizi na kwa sasa wanamkakati wa kuwasaidia ili kuondoa mlundikano wa kesi katika mahakama huku changamoto kubwa ikiwa ni kukosekana kwa mfumo wa kisheria wa kusimamia msaada kisheria.