Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki.
Mhe. Kairuki ameeleza hayo kwenye kikao cha wafanyakazi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala eneo la Segerea, jijini Dar es Salaam na kusema uhamisho lazima ufanyike endapo kukiwa na sababu za msingi sana.
“Baadhi ya waajiri wamekuwa na tabia ya kuwahamisha watumishi wa umma ambao wameonekana kuwa na tatizo na kuwahamishia sehemu nyingine, uhamisho wa namna hii haukubaliki tatizo la mtumishi linatakiwa kufanyiwa kazi kwenye kituo chake cha kazi na siyo kupeleka tatizo sehemu nyingine", amesema Waziri Kairuki.
Pamoja na hayo, Waziri Kairuki amewahimiza watumishi wa umma kubadili mtindo wao wa maisha ili kuweza kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi, kujiepusha na ugonjwa wa UKIMWI na magonjwa mengine yasiyokuwa ya kuambukizwa.



