
Pichani miili ikiwa eneo la makaburi ya pamoja.
Akizungumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Bwisya amesema kuwa kivuko kilizidisha abiria ambapo kilibeba watu na zaidi ya 260 na mizigo iliyozidi huku uwezo wake ni tani 25 pekee ambazo ni sawa na abiria 101 na magari matatu.
“Mimi nitaendelea kubaki Ukara ili kusimamia mazishi ya miili ya wataokuwa wanapatikana hadi hapo tutakapo hitimisha zoezi la uokoaji ikiwa tumefanikiwa kuokoa watu wote”, amesema Majaliwa.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema kuwa miili ambayo imeopolewa hadi leo mchana ni ya watu 224 ambapo wanawake wakiwa 125 na wanaume 71 watoto wa kike 18 watoto wa kiume 10, miili 7 bado haijatambuliwa.
Ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama Alhamis mchana Septemba 20, 2018 imefikia 224 huku uokoaji ukiendelea ambapo Rais John Magufuli ametangaza maombolezo ya siku nne na bendera za taifa zikiwa nusu mlingoti nchi nzima.