Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Waziri Mkuu aipa siku 2 Wizara ya Jafo

Alhamisi , 4th Feb , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameipa siku mbili Wizara ya TAMISEMI kufuatilia halmashauri za wilaya ambazo zilikuwa na makao makuu yake katika halmshauri za miji, kuhakikisha zinahamia kwenye makao mapya na zisipotekeleza apelekewe taarifa ofisini kwake Jumamosi Februari 6 saa 4 asubuhi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 4, 2021, Bungeni Dodoma, katika kikao cha Tatu, mkutano wa Pili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la mbunge wa Geita vijijini Joseph Musukuma, aliyehoji ni hatua gani zitachukuliwa kwa halmashauri ambazo zimekaidi agizo la Rais Magufuli, kwani wafanyakazi wake wanakwenda kulala mijini na kwamba wanazidi kuongeza gharama kwa serikali.

"Ni kweli Rais alitoa agizo na halmashauri nyingi zililitekeleza, nataka niagize halmshauri zilizotakiwa kuhama waondoke mara moja na wasipofanya hivyo mkuu wa mkoa husika achukue hatua dhidi ya watu hao ambao hawataki kwenda kwenye maeneo mapya", amesema Waziri Mkuu

Aidha Waziri Mkuu pia akaongeza"Naiagiza pia TAMISEMI kufuatilia kila halmshauri ambayo ilitakiwa kuhama na nitahitaji taarifa hizo Jumamosi ofisini kwangu saa 4:00 asubuhi ili nijue ni halmashauri gani watumishi hawajahama ili tuchukue hatua za kinidhamu kwa watumishi hao"

HABARI ZAIDI

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030