Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama
Kauli hiyo ameitoa leo 27 Julai 2023, alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea Shirika la Uvuvi la Nchini (TAFICO) Jijini Dar es Salaam, ambapo alisema (TAFICO) ni moja ya taasisi za serikali iliyopewa majukumu katika programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi lengo kubwa la kuongeza tija na faida katika mazao yatokanayo na kilimo na uvuvi.
Akizitaja Wizara na Tasisi zinazotekeleza programu hizo chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kuwa ni pamoja na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, (TAFICO) na (ZAFICO) Waziri Mhagama alitaka Taasisi hizo kuzingatia ubora, na thamani ya fedha katika mradi mzima.
"Natarajia kila senti itakayowekezwa katika mradi huu itaenda kujibu na kuleta matokeo halisi tena yakiwa chanya na yatakayosaidia nchi yetu kusonga mbele na kupata maendeleo endelevu kwa wananchi na Taifa kwa Ujumla," amesema Waziri Mhagama
Akizungumza katika Ziara hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi alisema, serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha kwamba nchi inanufaika na rasilimali maji hasa katika eneo la uvuvi, kupitia mradi wa (AFDP).