Jumatatu , 30th Oct , 2023

Waziri  wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth Gwajima amesema kuna haja ya kuweka mfumo maalumu katika fukwe ili huduma zinazotolewa kutambulika na watu wanaotoa huduma pia kutambulika lengo ni kuepuka watu matapeli ambao wanafanya ukatili

Dk Gwajima ameeleza hayo wakati alipofanya ziara katika fukwe za Coco na Kawe ili kujadiliana na watoa huduma za kuogelea (Beach boy) ikiwa ni hatua za kukomesha vitendo vya ubakaji kwa wasichana, vinavyofanywa na watu wachache wasiowaaminifu.

Nilichoona hapa ni kuwa hawa vijana wanahitaji kuweka mifumo maalum ya watu kujua huduma wanazotoa na nimewaagiza watoe matangazo na vipeperushi vya huduma ili wanaokuja hapa wasikutane na matapeli kwani hii inachafua taswira yenu,” amesema Gwajima