Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Waziri wa zamani wa sheria nchini China Bw. Fu Zhenghua, ambaye alikua  akiongoza mapambano ya kampeni dhidi ya rushwa  amekutwa na hatia ya makosa ya  rushwa.

 Bw. Fu amekutwa na hatia  mwezi Julai mwaka huu ,ya kupokea rushwa fedha za China Yuan milioni 117 ambazo ni zaidi yashilingi bilioni 38 za Kitanzania. 

Vyombo vya habari nchini humo vimesema kwamba  amehukumiwa hukumu ya kifo ambayo hata hivyo imesimamishwa ili kupisha mchakato wa kuifanya kuwa adhabu ya kifungo cha maisha ndani ya miaka miwili ijayo.   

Mashtaka yake yanakuja katika kipindi ambacho kuna mpasuko  kwenye mamlaka za nchi hiyo kuelekea mkutano muhimu sana wa chama tawala cha kikomunist mwezi ujao. 

Chama hicho tawala nchini China hufanya mkutano wake mkuu mara moja kwa miaka mitano, ambapo inatarajiwa kwamba Rais wa nchi hiyo  Xi Jinping ataongezewa muhula mwingine wa tatu madarakani, jambo abalo litakua historia kwenye nchi hiyo. Kesi ya Fu inafuatia ikiwa zimepita siku kadhaa maaskari watatu wastaafu wenye vyeo vikubwa nchini humo kuhukumiwa gerezani kwa makosa ya rushwa na kutohesimu kiti cha Rais   Xi.