Jumanne , 23rd Jun , 2020

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Musa Hassan Zungu ameagiza kusafishwa mara moja kwa eneo la Jangwani ambalo limezingirwa na vifusi vya mchanga vilivyotokana na miradi ya ujenzi.

Mussa Hassan Zungu

Ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara katika eneo hilo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

NEMC wametakiwa kuhakikisha eneo la Jangwani linasafishwa na kurudi katika matumizi yake ya kawaida kutokana na eneo hilo kuzingirwa na vifusi vya mchanga vilivyotokana na miradi mikubwa ya ujenzi na kuhatarisha 

Kwa upande wake Mkurugenzu wa Manispaa ya Ilala amesema kuwa kwa kushirikiana na NEMC watasimamia zoezi hiko ili kuhakikisha eneo la Jangwani linakuwa safi.