Jumanne , 23rd Jul , 2019

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, amewabeza viongozi mbalimbali wanaoonekana kuzikandamiza juhudi za maendeleo, zinazofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Waziri Mpina ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa Mkoani Simiyu, ameyabainisha hayo katika mkutano wa hadhara uliomkutanisha na wananchi jimboni kwake, ambapo amedai kuwa wanaondaa taarifa za kuleta mkanganyo kati ya Serikali na wananchi, hiyo nafasi haipo tena kwani wananchi wanakiona kinachofanywa na Serikali.

''Wananchi hawa wameteseka muda mrefu leo, Mh Rais kaweka misingi mizuri ya kudhibiti pesa za wananchi, sasa wengine wameanza kujitokeza na mawaraka yao, watayasoma wenyewe watanzania wako busy na maendeleo'' amesema Waziri Mpina.

Mpina ameongeza kuwa wananchi wanahitaji huduma bora za afya, bei nzuri ya pamba pamoja na huduma bora za kijamii, na kwamba wanaojitokeza leo na waraka pamoja na takwimu za uongo waachane na njama hizo zitakazopelekea kukivuruga chama.