Jumatano , 29th Apr , 2020

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani mkoani Iringa, ametoa msaada wa TV 40 ambazo zitawekwa katika maeneo ya wazi kwenye Vijiji 60 vya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ikiwa ni kuwasaidia wananchi wake kupata elimu ya kujikinga na maambukizi ya Corona.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Msaada huo umekabidhiwa na Katibu wake Tommy Malenga, kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela na kusema mbali na msaada wa TV hizo, pia vimetolewa vifaa kinga zikiwemo ndoo 270  za kunawia mikono kwa lengo la kuchochea ari ya wananchi kunawa mikono mara kwa mara.

"Tunataka na wananchi wetu walioko vijijini wanapata fursa ya kuangalia TV, hivyo tunakabidhi TV 40 na zitafungwa katika kila Kijiji kilichopo katika Jimbo la Isimani" amesema Katibu huyo.