Waziri amefikia uamuzi huo baada ya Mbunge wa Jimbo la Busega CCM Dkt Rhaphael Chegeni ambaye ametaka kauli ya serikali kuhusiana na ng'ombe ambao wanazuiliwa katika hifadhi hiyo.
''Mheshimiwa naibu spika ngombe wamezuiliwa wakati wao hawana akili na wanateswa bila malisho je serikali inachukua hatua gani ili wananchi wachukue mifugo yao?'' Ameuliza Dkt. Chegeni
Akijibu swali hilo waziri Maghembe amesema ng'ombe hao waachiwe mara moja ili kuleta mahusiano mazuri kati ya wananchi wanaozunguka hifadhi pamoja na serikali.





