
Baraza la Wazee Arusha limetaka ushirikishwaji katika vikao mbalimbali vya kijamii na ngazi za kimaamuzi ikiwemo Bungeni ili kutumia hekima na busara zao kwakuwa Wazee ni hazina.
Baraza hilo limemuomba Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo kupeleka kilio hicho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuteua uwakilishi wa Baraza la Wazee ndani ya Bunge.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Arusha Mzee Mhina Mbelwa wakati akizungumza kwenye hafla ya Uhamasishaji wa Kutoa Elimu ya Nishati Safi kwa Viongozi wa Baraza la Wazee Arusha.
"hatuna uwakilishi kuanzia ngazi za hususani Bungeni, makundi mengine yote wana uwakilishi lakini kwa bahati mbaya Uongozi wa Baraza la Wazee anayeingia pale kama Mbunge kutoka kwa Wazee hayupo wakati mwongozo unatutaka tupate uwakilishi, katika wale Rais anaowateua basi aangalie na wazee ili tupate uwakilishi"
Aidha, Mwenyekiti huyo ameiomba Halmashauri ya Jiji la Arusha kutambua uwepo wa Baraza la wazee