Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya CCM Abdallah Bulembo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo taifa Alhaji Abdallah Bulembo, amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati alipokuwa akiongelea masuala mbalimbali yanayoihusu Jumuiya hiyo likiwemo suala la mafanikio ya kielimu ambayo shule zilizo chini ya jumuiya hiyo imeyapata.
Aidha, kuhusu mafanikio katika sekta ya elimu, Bulembo amesema shule zilizo chini ya jumuiya zimefanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita mwaka huu ambapo mwanafunzi Idrisa Khamis kutoka shule ya sekondri ya Mwembetogwa mkoani Iringa ameibuka kuwa mmoja kati ya wanafunzi kumi bora kwa waliofanya mtihani huo.
Aidha, Bulembo amesema kuwa jumuiya hiyo pia imezima kile ilichokiita kuwa ni njama za kuanzishwa kwa mtandao wa utapeli wa fedha kama ule wa DECI, kupitia uanzishwaji wa taasisi ya kifedha ambayo ingejulikana kama Benki ya Familia.
Kwa mujibu wa Bulembo njama hizo za kuanzishwa kwa 'DECI' mpya kunafuatia wazo lililokuwepo hapo awali la mpango wa kunzishwa kwa benki hiyo.
Akitoa ufafanuzi kuhusu njama hizo, Alhaji Bulembo amesema jumuiya inafahamu umuhimu wa kutoa fursa za kiuchumi kwa wanachama wake na Watanzania kwa ujumla, lakini akatahadharisha kuwa kamwe Jumuiya hiyo haitakuwa tayari kuona njia chafu zinatumika katika kutimiza azma hiyo.




