Ijumaa , 9th Aug , 2024

Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kosa la mauaji ya dereva bodaboda aliyekutwa ameuawa Julai 24 katika Kijiji cha Stalike wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Kamanda wa PolisiMkoa wa Katavi Kaster Ngonyani

Kamanda wa PolisiMkoa wa Katavi Kaster Ngonyani, amesema baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilianza kufanya msako na hatimaye kuwatia mbaroni watuhumiwa hao. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodaboda mkoa wa Katavi Issack Daniel, amewaasa bodaboda kutokuwa na tamaa ya fedha pindi wanapotiliamashaka mienendo ya wateja wao.