Jumanne , 16th Jan , 2024

Wavuvi wawili wilayani Babati mkoani Manyara wamefariki dunia baada ya ngalawa waliyokuwa wakitumia kwenye shughuli za uvuvi ndani ya ziwa Babati kuzama asubuhi ya leo Januari 16, 2024 huku chanzo kikitajwa kuwa ni ulevi.

Ziwa

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea na juhudi za kutafuta miili ya wavuvi hao ndani ya ziwa hilo.

Taarifa zaidi zinafuata