MKUU wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza amewapa viapo vya utii wa kazi watumishi wa serikali TAMISEMI kwaajili ya kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili kuweza kuboresha elimu na kuondoka katika kundi la kuwa wa mwisho yaani kushika mkia.
Mahiza ametoa viapo hivyo wakati wa kikao na wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa, wakuu wa shule za sekondari na maafisa elimu ambapo ametoa agizo kwa wakuu wote wa shule za sekondari kuwa hadi kufikia tarehe 20 mwezi huu awe ameshapatiwa idadi kamili ya wanafunzi ambao wamefaulu kwenda sekondari na bado hawajaripoti mashuleni.
Sambamba na hayo pia amewataka walimu hao kuwa wabunifu mashuleni mwao kwa kuhakikisha wanatumia vizuri fedha zinazotolewa na serikali katika kuboresha mazingira ya shule na upatikanaji wa chakula kama alivyotolea mfano na kuipongeza shule ya wasichana ya Korogwe kwakuwa wanalima mazao yao ya chakula wenyewe shuleni hapo.



