Waziri wa TAMISEMI - George Simbachawene
Akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma, Simbachawene amesema watumishi hao wanatakiwa kuwa na utendaji unaojali matokeo na kuepuka utendaji wa mazoea, pamoja na kuzingatia nidhamu na utendaji wa watumishi wa umma.
Simbachawene amesema kumekuwa na tuhuma kwa baadhi ya watumishi kujihusisha na vitendo vya rushwa zikiwemo zinazohusiana na uhamisho, upangaji wa walimu na michakato ya teuzi mbalimbali na kuwa watumishi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Aidha, ametaka kila Idara na kitengo kuhakikisha kuwa zinapunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuelekeza rasilimali fedha katika kutekeleza majukumu ya msingi ambayo yataleta tija kwa taifa na kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu.






