
Usafiri wa Mtandaoni wa Uber
"Nauli elekezi iliyowekwa na mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini (LATRA) imesababisha changamoto kubwa kwa mifumo kama uber kuendelea kutoa huduma kwa wateja, hatutaweza kutoa huduma mpaka pale mazingira yatakapokuwa rafiki kwa sisi kuendelea kutoa huduma" - imeeleza sehemu ya ujumbe wa Uber kwa Wateja Wake.
Watumiaji wa Uber pamoja na madereva ambao Uber kwao ilikuwa ni ajira wamesema kuwa hatua hiyo itaathiri hali ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam hasa kwa watu wa kipato kidogo.
"Sisi watu ambao hatuna magari ndio tunaenda kuteseka kitokana na uber kusitisha huduma, uber wamekuwa wakitusaidia sana kufika tunapokwenda kwa haraka na hata bei yao ni nzuri. Ninaiomba LATRA wakae na serikali kuona namna ya kupunguza gharama kwasababu uber ni mwanzo tu, wengine pia kama Bolt watajitoa na wao" - Victoria Merikiadi, mtumiaji wa uber.
Aidha, hatua hii pia inetajwa kuathiri ajira kwa vijana waliokuwa wameajiriwa na uber kama madereva wake katika jiji hili la Dar es Salaam
"Sisi madereva wa Uber na Bolt hii ndiyo ofisi yetu, japo kipayo ni kidogo lakini tunapata riski ya kujikimu. Kwahiyo naiomba LATRA wafanye mazungumzo huduma irudi. Tutapoteza ajira" - Hamis Hamza, Dereva wa Bolt na Uber