Watuhumiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Arusha, Devotha Msofe, wakikabiliwa na mashitaka 16 likiwemo la mauaji ya Sudi Ramadhani.
Hata hivyo Hakimu Devotha Msofe aliwauliza watuhumiwa hao kama walishawahi kuomba kupatiwa hati hiyo, kwani kumbukumbu za Mahakama hazioneshi kama walishawahi kuomba kupatiwa hati.
Kwa upande wake Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Eliainenyi Njiro amesema kuwa, Sheria inasema upelelezi wa kesi ni siku 60 ila kama haujakamilika Mkuu wa Upelelezi (RCO) anaweza kuongeza siku 60, na iwapo upelelezi haujakamilika, sheria inamruhusu Mwanasheria wa Serikali kuongeza siku nyingine 60 kwa ajili ya upelelezi.
Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Julai 10 mwaka huu kutokana na upelelezi wake kutokukamilika.



