Alhamisi , 28th Mar , 2024

Watu wawili wameripotiwa kufariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea leo alfajiri ya leo Machi 28, 2024 ikihusisha mabasi mawili ya New Force, Sauli na lori la mafuta.

Picha ya ajali ya mabasi mawili na Lori la mafuta

Ajali hiyo imetokea eneo la Mlandizi karibu na JKT Club ambapo mabasi yameteketea kwa moto huku taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo zitatolewa lakini tayari Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboukabari Kunenge amewasili eneo la tukio. 

Aidha Tanki la mafuta la lori lililohusika kwenye ajali hiyo limelipuka wakati Jeshi la Zimamoto likiendelea kumwaga mafuta ili kuepusha madhara zaidi.