Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Watu wanataka chakula na siyo ndege - Rungwe

Alhamisi , 16th Mar , 2017

Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe Spunda ameishauri serikali kuweka mkazo zaidi katika kuhakikisha watanzania wanapa chakula, badala ya kuwekeza kwenye mambo mengine, ikiwemo ununuzi wa ndege.

Rungwe akiwa katika kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, amesema kwa sasa nchini hali ni mbaya, na watanzania wengi wanasumbuliwa na njaa huku maisha yakizi kuwa magumu, na kuikumbusha serikali kuwa ilipaswa kutengeneza vituo vya afya vya kisasa vyenye madawa ya kutosha pamoja na kuhakikisha mahitaji muhimu ya wananchi yanapatikana na siyo kutumia fedha za umma kununulia ndege na ujenzi wa reli za treni za umeme ambazo haziwanufaishi watanzania wa kawaida.

“Mimi sikosoi mambo anayoyafanya Mh. Rais , Pesa za ndege ingekuwa ni mimi ningetengeneza vituo vya afya vya kisasa, madawa yangepatikana kwa wingi lakini pia majiko katika shule ili watoto wanywe uji, Unatengeneza reli  unabebaba nini ? umekuwa kuli wa nchi zingine, watu wako hawana chochote cha kusafirisha kwenda kuuza huko Afrika Mashariki" Alisema Rungwe

Amebainisha kuwa ndege zilizonunuliwa na serikali hivi sasa hazipati abiria kwa kuwa watu wana njaa, huku akitolea mfano siku moja aliposafiri katika ndege hiyo "Mimi mwenyewe wala sijasimulia, nilipanda ndege kutoka Dar kwenda Arusha, abiria walikuwa 18 tu, yaani ndege ya abiria 98 lakini inaondoka na abiria 18, mimi mwenyewe nimeshuhudia"

Hashim Rungwe alipokuwa Kikaangoni 

Aidha Rungwe amesema vijana wa taifa wanapaswa kushiriki katika suala la uzalishaji wa chakula na siyo kutelekezwa mitaani kitendo ambacho kinawapelekea ushawishi wa kujiingiza katika matumizi ya uvutaji wa bangi.

Hata hivyo Rungwe amesisitiza kwamba wananchi wana njaa hivyo serikali inawajibu wa kuhakikisha chakula kinakuwepo kingi kwa kuwa hilo ndilo jukumu lake hasa ikizingatiwa kwamba wananchi wanalipa kodi.

“Matatizo makubwa tuliyo nayo sisi nchini ni uongozi tu,  anayekusanya kodi ndiye mwenye kupanga pesa itumike vipi. Huwezi ukamwambia mtu akalime wakati hana vifaa atatumia mawe? Arudi kwenye stone age? Vijana wanaingia kwenye madawa kwa kukosa shughuli za kufanya". Kauli ya Rungwe

Rungwe amesesema yeye angepatiwa nafasi ya kuongoza taifa la Tanzania kipaumbele cha kwanza kutoka kwake kingekuwa ni chakula ili wananchi waone tija ya kuishi kwenye nchi yao.

Akijibu swali kuhusu hali ya elimu nchini, Rungwe amesema elimu ya Tanzania inakwamishwa na njaa, hasa hasa kwa wanafunzi na walimu, huku akishauri uwekwe utaratibu wa kutoa chakula mashuleni.

Huyu hapa Rungwe.....

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali