Jumatatu , 24th Oct , 2016

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema watu milioni 47 wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya Matende, Ngiri Maji na Kichocho nchini Tanzania huku wengine milioni 6 wakiwa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa usubi.

Afisa Mipango katika mradi wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele kitaifa Bw. Oscar Kaitaba

 

Takwimu hizo zimetolewa leo na Afisa Mipango katika mradi wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele kitaifa Bw. Oscar Kaitaba wakati akielezea jitihada ambazo zimeanza kuchukuliwa na serikali za kuhakikisha inazuia magonjwa hayo.

Amesema kama wananchi hawatafuata taratibu za kitaalamu zinavyoelekeza madhara zaidi yanaweza kutokea hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuzingatia taratibu za afya.