Alhamisi , 4th Feb , 2016

Watoto wenye ulemavu wa kuota nundu mgongoni ambao ni wakazi wa kijiji cha Namba Nne wilaya ya Arusha, wameanza kupatiwa matibabu katika hospitali ya Seliani mara baada ya daktari mmoja kujitolea kuwasaidia matibabu.

Dkt. Catherine Mung`ong`o,Mtaalamun wa Upasuaji wa watoto

Akizungumza hospitalini hapo Dkt. Catherine Mung`ong`o ambaye ni mtaalam wa upasuaji wa watoto, amesema kuwa watoto hao wanakabiliwa na upungufu wa madini ya Folic Acid na Calcium mwilini ambayo husababisha mifupa kuwa dhaifu na kujikunja kama ilivyojikunja mgongoni na kusababisha ugonjwa ambao kitaalam unaitwa Caifosis

Dkt Catherine amesema kuwa iwapo tatizo hilo lingejulikana mapema wakiwa wadogo wangeweza kuwafanyia upasuaji ila kwa sasa, watawapatia vitamin hiyo pamoja na mazoezi ili waweze kuimarika na si kudumaa kama ilivyo awali

Kwa upande wake Mama Mzazi wa watoto hao Theresia Ezekiel na Diwani wa Kata hiyo Ojwaan Salekwa aliyewafikisha hospitalini hapo ametoa wito kwa watanzania kujitoa kuwasaidia watoto hao kwa hali ili waweze kusomeshwa na kupata matibabu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu tukio hili, baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wameiomba serikali kutoa elimu ya uzazi hasa maeno ya vijijini ili kuepukana na matatizo ya kiafya yanayowakumba wanawake na watoto.

Watoto hao ni Jeremia Ezekiel, Musa Ezekiel, Goodluck Ezekiel na Elia Ezekiel wenye umri wa kati ya miaka 19 na miaka miwili.