Jumatatu , 29th Nov , 2021

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, amesema kwamba awali Uganda alizuia kabisa taasisi ama shule yoyote kuitwa kwa jina lake, isipokuwa mke wake na watoto wake licha ya kwamba wapo baadhi ya watoto wake waliokataa kutumia jina lake.

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni,

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 29, 2021, Chato, Geita, wakati akikabidhi shule aliyoijenga kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, iitwayo Museveni shule ya Msingi, itakayochukua wanafunzi kuanzia ngazi ya awali, darasa la kwanza hadi la saba.

"Hii ni mara ya kwanza duniani kupata kituo au taasisi inayoitwa Yoweri Museveni, haikuwepo kwa sababu nilipinga kabisa sitaki jina langu kukaa kwenye vitu vya watu, mimi niko na ng'ombe zangu na watoto wangu waliokubali kulitumia sababu kuna baadhi walikataa kutumia jina langu, ila ndugu zangu Watanzania wameamua sipingi," amesema Rais Museveni.