Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt.Sirilla Mwanisi.
Akizungumza na East Africa Radio Dkt. Mwanisi amesema, athari za kukosekana kwa chanjo hiyo ni pamoja na ubongo wa mtoto kudumaa, uoni hafifu pamoja na kuzorota kwa hali ya ngozi ya mtoto, inayopelekea tatizo la kutojiamini na hivyo kushindwa kufanya vizuri katika masomo.
Aidha Dkt. Mwanisi amesema kuwa ugonjwa wa minyoo ni jambo lisiloepukuka hasa kwa mtoto kuanzia miezi sita hadi miaka mitano hivyo kupata chanjo ni bora zidi kutokana na madhara ya minyoo kuwa makubwa katika makuzi ya mtoto.
Amesema kuwa serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa watoto wote kuanzia umri mwa miezi sita na kuendelea wanapata huduma hiyo ya chanjo ya ugonjwa wa minyoo.
Kwa upande wake mratibu wa zoezi la chanjo kitaifa la matone ya Vitamin A linalokwenda sambamba na ugawaji wa dawa za minyoo Dkt. Alex Mkamba, amesema zoezi hilo limekuwa likilega lega kutokana na ushiriki mdogo wa wananchi na kuwataka wenyeviti wa serikali za mitaa kuunga mkono zoezi hilo ili kufikia malengo ya asilimia 85 yaliyowekwa na serikali.