Alhamisi , 29th Sep , 2022

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, imefanikiwa kuwawekea vifaa vya usikivu watoto saba na kufanya idadi ya watoto waliofungwa vifaa vya usikivu kutoka mwaka 2017 kufikia 56.

Vifaa vya usikivu

Watoto hao ambao kabla ya kufungwa vifaa hivyo walifanyiwa upasuaji chini ya jopo la madaktari  wa kitanzania huku wakipata hisani ya vifaa kutoka kwa wahisani bado huduma hiyo imekuwa ikigharimu shilingi milioni 40 pungufu ya shilingi milioni 60 endapo wangetibiwa nje ya nchi.

Aidha Profesa Mselu amesema watoto hao kwa asilimia kubwa gharama za matibabu ni msaada kutoka Muhimbili na kampuni ya vifaa vya masikio earkit kupitia utaratibu uliowekwa na Muhimbili kuanzia mwaka 2017.

Kwa upande wake mmoja wa wazazi ambao mtoto wake amenufaika na huduma hiyo amesema huduma hiyo imesaidia kuleta matumaini mapya kwa watoto ambao awali walikosa furaha kutokana na shifa ya usikivu.