Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Charles Mahera
Mapema hii leo Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Charles Mahera wakati akizindua kikao kati ya tume ya uchaguzi na watoa huduma ya habari mitandaoni amewataka pia kutumia kalamu zao kulinda amani iliyopo huku akionya kuwa tume inawauwezo wa kuwachukulia hatua wadau wa uchaguzi wasiozingatia mioangozo ya maadili iliyosainiwa.
Aidha, vijana wametakiwa kujiajiri kwenye sekta hiyo huku wakizingatia kuheshimu taratibu za usajili zilizowekwa na mamlaka mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) huku wakikumbushwa jinsi NEC inavyoendelea kuweka uwanja sawa kwa washiriki wote wa uchaguzi mkuu ujao. Ambapo baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema yamekuja katika wakati mzuri.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema lengo la kikao hicho kwa watoa huduma ya habari mitandaoni ni kuongeza kukumbushana kuwa kuna maisha mengine baada ya uchaguzi mkuu hivyo ni muhimu kutumia lugha yenye staha kipindi chote cha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 28,2020.