Jumatano , 27th Jul , 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa uwepo wa nyumba za walimu ni moja ya vivutio vya walimu kwenda kufanyakazi mahali popote.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene

Waziri Simbachanwene amesema hayo Mjini Songea Mkoani Ruvuma, alipokutana na watendaji mbalimbali kwa lengo la kujionea namna ya wanavyofanya kazi katika maeneo yao.

Waziri Simbachawene amewataka watendaji hao kuweka mikakati ya uboreshaji wa mazingira ya walimu ili waweze kutoa elimu bora na kunyanyua sekta ya elimu nchini.

Aidha Mhe Simbachawene amewataka watendaji ambao wanalaumiwa kuwachelewesha walimu pindi wanapokwenda kufuata huduma muhimu mijni na kutaka kuwashughulikia haraka ili wakatimize majukumu yao kwa ufanisi.

Aidha Mhe. Simbachawene amewataka Wakurugenzi wa sasa kuacha kuwa miungo watu na badala yake wajitoe katika kushughulikia kero mbalimbali ikiwemo changamoto wanazokumbana nao walimu.

Sauti ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene,