Alhamisi , 9th Jul , 2015

Serikali imewataka watendaji wakuu wa serikali kupata mafunzo maalum ya namna ya kuendesha shughuli za mamlaka ya serikali za mitaa ili kujua jinsi ya kuendesha shughuli hizo bila kusababisha migongano.

Waziri wanchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Hawa Ghasia

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia wakati akizindua bodi mpya ya chuo cha serikali za mitaa kilichopo Hombolo katika Manispaa ya Dodoma.

Amesema mara nyingi kumekuwepo na migongano ya kiutendaji kwa watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa kutokana na kutokujua majukumu yao na mipaka yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti mstaafu wa bodi hiyo, Ramadhani Khalfan alisema changamoto kubwa inayokikabili chuo hicho ni ufinyu wa bajeti ambao unakwamisha mipango mingi wanayojiwekea katika kufikia malengo yao.