Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Dismas Disusi akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwakwe Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Dismas Disusi amesema tukio hill limetokea usiku wa tarehe 26 mwezi huu ambapo mwalimu huyo alikuwa anatoka katika ofisi yake ya biashara.
Aidha Kaimu Kamanda amesema uchunguzi utakapokamilika watu hao watafikishwa Mahakamani ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wengine ambao wamehusika katika kutenda kosa hilo