Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku,
Akizungumza katika mdahalo ulioandwaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Joseph Butiku amesema kuwa lengo la kuendesha mdahalo huo ni kuwakumbusha vijana jinsi ya kutunza amani na kuvumiliana kutoana na mihemko ya kisiasa.
Mh. Butiku ameongeza kuwa mdahalo huo ulikua ni kuhakikisha maadili mema yanafuatwa ,amani inatawala na kuwataka vijana kuchambua sera za vyama na kuacha kuongozwa na viongozi wazee ambao wanawatuma kufanya mambo ambayo yanakikuka sheria za nchi.
Kwa upande wake aliyekuwa mjumbe wa iliyokuwa tume ya kukusanya Maoni ya Katiba Mpya Bw. Hamphery Polepole amesema kuwa watanzania wafuate maneno ya baba wa taifa kuwa utajiri usiwe kigezo cha urais.
Naye aliekuwa Rais wa Bunge la Afrika mama Getrude Mongela amewataka vijana kujua sera za kila chama na kuchagua chama kutokana na muelekeo wa sera zake na siyo kwenda kwa kufuata upepo wa chama huku akiwataka vijana wengi zaidi kujitokeza katika kuiongoza nchi.