Jumanne , 11th Nov , 2014

Watanzania wenye uwezo wametakiwa kuwekeza kwenye sekta ya kilimo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuyaongezea thamani mazao na kupunguza upatikanaji masoko kwa wakulima na kuongeza ajira kwa wananchi ndani ya EAC.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu.

Akiongea jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu amesema Changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni viwanda vya kusindika mazao hivyo endapo watajitokeza wawekezaji katika eneo hilo itasaidia kupunguza upotevu wa Chakula.

Aidha Dk. Nagu amewapongeza wakulima nchini kwa kuzalisha chakula kwa wingi kwa mwaka ambapo kwa mwaka huu pekee serikali ya Tanzania imenunua Tani 280,000 kwa ajili ya kuhifadhi ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na balaa la njaa.

Kwa upande wake mkurugrnzi wa kiwanda cha kusaga nafaka cha Basic Element, Leornard Rubuya amesema wamekuwa wakikusanya hadi tani laki moja za nafaka kila mwaka kutoka kwa wakulima na kuyasindika.