Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania Mh. George Simbachawene.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishasti na Madini nchini Tanzania Mh. George Simbachawene mara baada ya kuzindua shahada ya uzamili ya sayansi ya mafuta na gesi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Aidha, Mh. Simbachawene amevitaka vyuo vinavyofundisha elimu ya mafuta na gesi nchini kufanya utafiti wa kutosha ili wawekezaji wanapokuja wakute tafiti za kutosha zilizofanywa na nchi kabla ya tafiti zao.
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala amesema kuwa chuo kimejipanga kutatua changamoto zote na kuzalisha wasomi wenye uwezo unaohitajika na soko la mafuta na gesi nchini.