
Wito huo umetolewa na mdau wa utalii nchini Bi. Nangasu Warema wakati akihitimisha kampeni ya serikali ya kuvutia wawekezaji kupitia kutangaza vivutio hivyo iitwayo 'Talii na Mama Samia'.
Bi. Werema amesema katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka ni fursa kwa wananchi kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio na hifhadhi mbalimbali ikiwemo kisiwa cha Saa nane kilichopo Jijini Mwanza.
Inaelezwa kuwa zoezi la kutangaza vivutio vya utalii nchini ni muendelezo wa jitihada za Serikali kupitia Filamu ya 'The Royal Tour' iliyowezesha kupatikana wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.