Jumatano , 23rd Nov , 2022

Nsamaka Masanja ambaye ni mama mzazi wa Gift Amani mwenye umri wa miaka mitatu, mwenye uvimbe maeneo mbalimbali ya mwili wake amewaomba watanzania kumsaidia ili aweze kumudu malezi ya mwanaye.

Mtoto Gift Amani na mama yake

EATV imefika mitaa ya Muhimbili jijini Dar, na kukutana na binti Gift ambaye alifika hospitali ya Taifa Muhimbili kufanyiwa matibabu akieleza kuwa mtoto wake alizaliwa na uvimbe maeneo mbalimbali ya mwili wake, kiwa pamoja na mikononi, kifuani na makwapani, huku ikiendelea kukuwa kadiri siku zinavyoendelea.
 
Akiendelea kuzungumza kwa Uchungu mkubwa, Mama Gift anabainisha kuwa baada ya kuhangaika kupata matibabu ya afya ya mtoto wake, amefanikiwa kufika hospitali ya Taifa Muhimbili, na haya ndio majibu aliyopewa.

Na hapa anaeleza uhitaji mkubwa alionao kwa sasa, huku akiomba zaidi msaada kwa ajili ya mtoto wake kuwezwa kupata elimu.

Kwa yoyote atakayetaka kumsaidia Gift na mama yake, anaweza kusiliana zaidi kwa namba 0759665555