Jumapili , 14th Jun , 2020

Raia takribani 60 wa Tanzania waliokwama Afrika Kusini kutokana na zuio lililowekwa la kutoka au kutosafiri nje ya nchi hiyo kutokana na mlipuko wa COVID-19, wamerejea nchini leo Alfajiri wakitokea Johannesburg.

Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere

Raia hao wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam, saa 10:10 Alfajiri kwa ndege maalum iliyotumwa nchini humo kuwachukua.

Wameruhusiwa kuondoka nchini Afrika Kusini baada ya kukidhi vigezo na kukubaliwa kuondoka nchini humo.

Tazama hapa walivyotua Uwanja wa Ndege wa JNIA.