Ijumaa , 25th Mar , 2016

Waziri wa maliasili na Utalii amewasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi watumishi watano wa wizara hiyo akiwemo Mkurugenzi Msimamizi wa Idara ya wanyamapori Dkt. Charles Mlokozi kwa kosa la kutoa vibali vya kusafirisha tumbili kwenda nchini Albania.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe,

Hatua hiyo inakuja wakati Jeshi la Polisi limekamata raia wawili wa Uholanzi katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA), wakiwa wanataka kusafirisha tumbili hai 61 kwenda nchini Albania.

Akiongea na Waandishi wa Habari Jana Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, akatangaza kusimamishwa kazi kwa watumishi hao kutokana na kukiuka maagizo yake na kuisababisha serikali hasara.

Katika hatua nyingine Waziri Maghembe ametangaza watumishi wengine watakaokaimu nafasi za Watumishi hao waliosimamishwa kazi mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.

Aidha Prof. Maghembe amethibitisha kukamatwa kwa tumbili hao 61 Mkoani Kilimanjaro waliokuwa wakisafirshwa kinyume cha taratibu ambapo amesema watu hao wa ulaya mashariki walikodisha ndege kwa ajili ya kuwasafirsha tumbili hao.