Ijumaa , 5th Aug , 2016

Serikali imezitaka taasisi za elimu ya juu nchini kuweka mifumo itakayowasaidia kuwaandaa kitaaluma wanawake ili waweke kuwa wafanyakazi bora wanaoajirika na kujiajiri.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama,

Hayo yamezungumzawa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakati akifungua mkutano mkuu wa tatu wa kamati ya Chama cha Wanawake Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu juu nchini(THTU)unaofanyika jijini Mwanza.

Waziri Muhagama amesema kuwa hatua hiyo italiwezesha taifa kufikia uswa wa Kijinsia katika nyanja zote za kimaendeleo nchini na kuwa chachu ya kukuza uchumi wa nchi mpaka ifikapo mwaka 2030.

Mhe. Muhaga amesema kuwa wanawake wanakumbana na changamoto nyingi wakiwa makazini ikiwemo wakiwa katika malezi ya watoto wachanga wakati wakiwa kazini wengi wanakosa muda wa kufanya mambo yote mawili kutokana na kukosa muda kutoka kwenye maofisi yao.

Sauti ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama,