Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akimtwika maji mama katika Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi.
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka wizara ya Maji na Umwagiliaji, Joseph Makungu, amesema mfumo utawezesha kufanya maamuzi stahiki na kwa wakati katika eneo la Mradi kuliko ilivyokua hapo awali.
Bw. Makungu amesema moja kati ya Changamoto zilizokuwa zinawakabili hapo awali ilikua ni pamoja na ucheleweshaji wa Takwimu kutoka maeneo tofauti ya nchi hali iliyokuwa inawafanya wafadhili nao kuchelewa kutoa fedha za kumalizia miradi hiyo.
Kwa upande wako Washiriki wa Mafunzo hao wamesema kwa kiasi kikubwa mfumo huo mpya utawasaidia kuanzisha miradi mingi zaidi kwa kuwa takwimu zitakua zinafika kwa wakati hivyo miradi mingi kuisha kwa wakati.



