Jumanne , 15th Nov , 2016

Serikali imeagiza idara ya uhamiaji nchini kufanya uhakiki upya wa vibali vya wahamiaji wote walioko nchini na kwa wale ambao hawana sifa zinazostahili warudishwe kwenye nchi zao kwakuwa wanaishi nchini kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akikagua utendaji kazi wa wafanyakazi wa uhamiaji nchini.

 

Agizo hilo limetolewa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba alipokutana na viongozi wa idara ya uhamiaji nchini kwaajili ya kujadili na kutatua kero mbalimbali katika idara hiyo.

Kwa upande wa mifumo ya utoaji vibali Mhe. Mwigulu ameagiza idara hiyo iunde tume maalum ya kujadili nakuangalia namna ya kuweka mifumo maalum ya kutoa vibali vya uraia kwa urahisi ili kupunguza malalamiko na ufisadi ambao kama hautatatuliwa mapema utasababisha hasara kwa taifa.

Aidha amewaagiza watawala katika idara hiyo kutenda haki kwa watumishi wake na watanzania kwa ujumla sambamba na kuwalipa madeni yao watumishi wapya walioajiriwa na idara ya uamiaji nchini.