Wasanii nao wamo uteuzi wa Rais Samia

Jumapili , 20th Jun , 2021

Katika majina mbalimbali ya Wakuu wa Wilaya walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  wasanii pia wamepata nafasi.

Kulia ni Nickson John maarufu kama Nikk wa Pili ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe pamoja na Juma Chikoka maarufu Chopa Mchopanga, Mkuu wa Wilaya mteule wa Rorya mkoani Mara.

Miongoni mwa wasanii walioteuliwa ni Nickson John maarufu kama Nikk wa Pili ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Aidha Rais amemteua muigizaji Juma Chikoka maarufu Chopa Mchopanga, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Kutoka tasnia hiyo ya sanaa Rais Samia pia amembakiza Jokate Mwegelo ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe sasa amehamishiwa Wilaya ya Temeke Dar es salaam.

Soma orodha kamili hapo chini.