Jumapili , 8th Sep , 2019

Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba,  amezungumza namna alivyokuwa anamfahamu marehemu Robert Mugabe,  ambapo amemtaja kuwa ni miongoni mwa alama za viongozi wa Afrika ambao walipigania uhuru wa nchi zao, licha ya kupitia mateso makubwa kutoka

Jaji Joseph Sinde Warioba

kwa makaburu.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital leo Septemba 8, 2019, Jaji Warioba amesema kuwa licha ya wengi kuiona Zimbabwe haiko sawa kwa kipindi hiki, lakini ni kiongozi pekee aliyeitoa Zimbabwe katika wakati mgumu wa masuala ya ubaguzi wa waafrika kutothaminiwa na kuweka usawa wa kibinadamu.

''Ni kweli sasa hivi Zimbabwe ina matatizo lakini siyo peke yake yanatokea, Mugabe kama kiongozi pamoja na yote yaliyotokea hakuna atakayebisha kwamba alikuwa ni mmojawapo wa viongozi imara waliojua kupigania haki, na alipopata uongozi alijitahidi kuifanya Zimbabwe iwe mahali ambapo watu wote wanaishi sawa'' amesema Jaji Warioba.

Akizungumzia masuala ya ardhi ya Zimbabwe Jaji Warioba  amesema, wazungu wengi walipora ardhi kubwa na yenye rutuba na kuwaachia wazawa maeneo madogo na hiyo ndiyo imekuwa chanzo cha matatizo ya sasa na kuomba  suala hilo lipatiwe ufumbuzi kwa kuaminini kwamba Zimbabwe itatulia.