
David Silinde,
Wakichangia bajeti hiyo, wabunge walio wengi wamelalamikia kitendo cha serikali kuondoa msamaha wa kodi katika kiinua mgongo chao wanachopaswa kulipa baada ya miaka mitano.
Wamedai kuwa haina maana yoyote kwa maamuzi hayo kufanyika sasa wakati malipo ya kiinua mgongo hicho yanafanyika baada ya miaka mitano yaani 2020 hivyo ingepswa kujumishwa katika bajeti ya mwaka 2020/21 badala ya bajeti ya 2016/17.
Pia wamedai kuwa pesa hizo hazipaswi kukatwa kodi kwa kuwa ndiyo tegemeo pekee la wabunge katika maisha baada ya kumaliza kipindi chao cha ubunge.
"Mh Waziri sisi wabunge tuna hali ngumu, huko majimboni kwetu sisi ndiyo ATM za wananchi, mnatukata kodi katika mishahara yetu ya kila mwezi, halafu hata hiki kiinua mgongo tunachotegemea nacho mnataka kikatwe kodi, hatutakubali, hatutakubali" Alisema Kangi Lugola katika mchango wake.
Kuhusiana na makato hayo, kambi rasmi ya upinzani imetamka kuyaunga mkono na kuitaka serikali iende mbali zaidi kwa kuondoa kuondoa kabisa posho za wabunge kwa madai kuwa mishahara yao inawatosha.
Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh David Silinde alisema kuwa kama kweli serikali ina dhamira ya dhati ya kubana matumizi, inapaswa kuweka usawa kwa wananchi wote kwa kuondoa posho zote zisizo na ulazima zikiwemo za wabunge.
Pia Silinde amesema serikali inapaswa kukata kodi katika mapato yote ya viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu n.k